NewsSWAHILI NEWS

Waziri mkuu Slovakia aliyepigwa risasi arudi kazini na mkongojo

Bratislava, Slovakia. Waziri Mkuu wa Slovakia, Robert Fico amerejeaa kazini, ikiwa ni karibu miezi miwili baada ya kupigwa risasi hadharani.

Ilikuwa Mei 15, 2024 ambapo Waziri huyo Mkuu alipigwa risasi nne na mtu aliyekuwa katikati ya umati aliyokuwa akisalimiana nao baada ya kutoka kwenye mkutano.

Baada ya tukio hilo Fico mwenye umri wa miaka 59 alifanyiwa upasuaji wa muda mrefu katika hospitali iliyo karibu. AFP imeandika.

Baadaye vyombo vya usalama vilimtambua aliyetekeleza jaribio hilo la mauaji ni mshairi aitwaye Juraj Cintula mwenye umri wa miaka 71 alifunguliwa mashtaka ya ugaidi huku akiwa rumande akisubiri hukumu.

Taarifa zinasema wakati Fico akichukua madaraka ya uwaziri mkuu, nchi yake ya Slovakia ilikataa kuendelea na msaada wa kijeshi kwa Ukraine, inayokabiliwa na uvamizi wa Urusi tangu Februari mwaka 2022.

Fico alitolewa hospitalini Mei 31 na alijitokeza hadharani kwa mara ya kwanza kwenye sherehe karibu na mji wa Bratislava Ijumaa iliyopita.

Awali, Waziri Mkuu, Fico alipigwa risasi alipokuwa katika mji wa Handlova baada ya kuondoka kwenye mkutano, ingawa alikuwa katika hali mbaya lakini alifanyiwa upasuaji afya yake inaimarika japokuwa moja kati ya risasi alizopigwa ilipenya tumboni.

Tukio hilo liliwashangaza maofisa usalama wa Fico, ambao picha zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ziliwaonyesha wakimbeba na kumuingiza kwenye gari, kisha kuondoka eneo la tukio.

Kutokana na tukio hilo, Rais wa Marekani, Joe Biden alisema: “Tunalaani kitendo hiki cha kutisha na cha ukatili. Ubalozi wetu unawasiliana kwa karibu na Serikali ya Slovakia na uko tayari kusaidia,” alisema katika taarifa ya Ikulu.

Related Articles

Back to top button
Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker!