NewsSWAHILI NEWS

Shahidi kesi ya mkopo tata wa Equity kikaangoni siku nne mfululizo

Dar es Salaam. Kesi ya mgogoro wa malipo ya mkopo inayozikabili Benki za Equity Tanzania (EBT) na Equity Kenya (EBK), Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara, Dar es Salaam sasa itaunguruma kwa siku nne mfululizo kuanzia Septemba 2 mpaka 5, 2024.

Kwa siku hizo zote shahidi wa pili wa upande wa madai atakuwa katika kikaango cha maswali ya dodoso kutoka kwa mawakili wa utetezi katika kesi hiyo.

Kesi hiyo imefunguliwa na Kampuni ya Continental Reliable and Clearing (CRC) (mkopaji) dhidi ya benki hizo (mkopeshaji), ikipinga kudaiwa kurejesha mkopo huo wa zaidi ya Dola za Marekani 10.13 milioni ilizokopeshwa na benki hizo.

Kwa sasa kesi hiyo iko katika hatua ya usikilizwaji, ambapo Mahakama hiyo inaendelea kupokea ushahidi wa upande wa mdai (CRC), na sasa ikiwa inaendelea kupokea ushahidi wa shahidi wa pili wa madaii.

Kesi inayosikilizwa na Jaji Profesa Agatho Ubena ilipangwa kuendelea mahakamani hapo leo Jumanne Julai 9 na kesho Jumatano Julai 10, 2024.

Hata hivyo kwa leo imekwama kwa kuwa Jaji Ubena anayesikiliza hayupo, badala yake imeahirishwa na Naibu Msajili wa Mahakama hiyo Joyce Minde, hadi tarehe hizo.

Kesi hiyo ilipoitwa kwa Msajili kwa ajili ya ahirisho hilo, wakili wa mdai, Frank Mwalongo ameomba wapangiwe kuendelea siku ya kesho Jumatano lakini Naibu Msajili Minde amesema hata kesho Jaji Ubena hatakuwepo, ndipo Wakili Mwalongo akaiomba hizo tarehe za Septemba.

CRC ilifungua kesi hiyo baada ya benki ya EBK kupitia wakala wake, EBT kuiandikia barua ikiipa siku 21  kurejesha mkopo wake uliotolewa kwake kwa nyakati tofauti kuanzia mwaka 2013, Dola za Marekani 10,139,664.95 (yaani Dola 10.13 milioni, sawa na zaidi ya Sh26 bilioni).

Kesi hii ni miongoni mwa kesi kadhaa zilizofunguliwa na kampuni mbalimbali zikipinga kudaiwa na benki hizo na zile zilizofunguliwa na benki hizo dhidi ya kampuni kadhaa zikizidai kampuni mbambali pesa ambazo zinadai zilizikopesha mabilioni ya fedha, lakini zimeshindwa au zimepuuza kurejesha mikopo hiyo.

Katika kesi hiyo ya kibiashara namba 16 ya mwaka 2023 inayosikiliizwa na Jaji Profesa Agatho Ubena, CRC inadai kuwa ilisharejesha mkopo wote na hivyo haina deni kwa benki hizo.

Mara ya mwisho Mahakama hiyo iliikatalia kampuni hiyo kupokea nyaraka muhimu katika utetezi wake kutoka na kutokutomiza matakwa ya kisheria.

Kampuni hiyo kupitia shahidi wake wa pili, Alexander Gombanila akiongozwa na Wakili wa kampuni hiyo, Mwalongo, iliiomba mahakama hiyo ipokee nyaraka hiyo iliyodaiwa kuwa ni jedwali la malipo ya mkopo wote ambao kampuni hiyo ilipewa na benki hizo.

Hata hivyo mawakili wa benki hizo, Emmanuel Saghan anayeiwakilisha EBT (mdaiwa wa kwanza) na Mpaya Kamala, anayeiwakilisha EBK (mdaiwa wa pili) walipinga nyaraka hiyo kupokewa wakidai kuwa haijakidhi matakwa ya kisheria.

Mahakama katika uamuzi wake ilikubaliana na hoja za pingamizi la mawakili wa utetezi ikaitupilia mbali nyaraka hiyo.

Baada ya hatua hiyo mawakili hao wa utetezi walianza kumhoji shahidi hugo maswali ya dodoso kuhusiana na ushahidi wake aliokwishauwasiliaha mahakamani hapo kwa njia ya maandishi pamoja na nyaraka mbalimbali wanazokusudia kutumika kama vielelezo vya ushahidi.

Aliyeanza kumhoji shahidi huyo ni Wakili Saghan ambapo pamoja na mambo mengine shahidi huyo alieleza kuwa yeye hakuwepo wakati mkopo huo inatolewa kwani alikuwa bado hajaajiriwa katika kampuni hiyo.

Badala yake alidai kwamba taarifa alizozitoa kuhusiana na mkopo huo ni zile alizozisikia kwa wafanyakazi wenzake na alizozikuta ofisini. Hata hivyo hakumaliza maswali yake ndipo kesi hiyo ikaahirishwa mpaka leo na kesho.

Sehemu ya mahojiano hayo ilikuwa kama ifuatavyo

Wakili Saghan: Shahidi, jana ulikula kiapo hapa kabla ya kutoa ushahidi wako, unajua maana ya kile kiapo?

Shahidi: Ili kuongea ukweli

Wakili: Nani alikutengenezea hiyo statement?

Shahidi: Niliitengeneza mwenyewe nikiongozwa na mwasheria

Wakili: Unaweza kumkumbuka huyo mwanasheria?

Shahidi: Ni Wakili Mwalongo

Wakili: Unamaanisha nini kusema alikuongoza? aliyeidraft ni wewe au nani?

Wakili: Kwa hiyo mwanasheria wako alikuongoza kufanya nini?

Shahidi: Katika kufanya final touches (marekebisho ya mwisho) kwamba hiki ndicho kinastahili kuwasilisha mahakamani

Wakili: Final touches unamaanisha nini, nini kiliongezwa au kilipunguzwa?

Shahidi: Kwamba unaiandikaje ili iwe ushahidi lakini kwamba kutoa taarifa mimi ndio chanzo.

Wakili: Unakumbuka wakati unasaini hiyo statement nani alikuwepo?

Shahidi: Nakumbuka alikuwepo Mwalongo.

Wakili: Ulianza kazi Continent Reliable Clearing mwaka gani?

Shahidi: Mwishoni mwa mwaka 2022.

Wakili: Unakumbuka mkopo wa mwisho kutolewa kwa CRC ilikuwa mwaka gani?

Shahidi: Kwa taarifa nilizozikuta ilikuwa Novemba 2021.

Wakili: Kwa hiyo ni sahihi wewe hukuwahi kuhusika katika uombwaji wa mikopo ambayo Iko katika migogoro kwenye hii kesi?

Wakili: Kwa hiyo ni sahihi pia kuwa wewe uliambiwa tu kuhusu hii mikopo ambayo iko kwenye mgogoro kwenye hii kesi?

Wakili: Ulishuhudia utolewaji au upokelewaji wa hii mikopo yote?

Wakili: Haukuwepo wakati inatolewa maana yake uliambiwa kwamba ulikuwepo ilitolewa na ukapokewa, si ndio?

Wakili: Hebu tuambie wewe unaijua hii mikopo kutokana na kuambiwa au kwa ufahamu wako mwenyewe?

Shahidi: Nilipata taarifa nilizozikuta ofisini.

Wakili: Kuna mtu mwingine ambaye alikuwa taarifa hizi?

Wakili: Huyo mtu aliyekupa hizo taarifa anaitwa nani?

Shahidi: George Bishashara

Related Articles

Back to top button
Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker!