NewsSWAHILI NEWS

Pete janja kuingia sokoni Julai 24

Dar es Salaam. Miaka kadhaa tangu dunia ianze matumizi ya simu janja na baadaye saa janja, teknolojia mpya ya pete janja ‘smart ring’ itakayokuwa na uwezo wa kufuatilia afya ya mvaaji na mengineyo inatarajiwa kuingizwa sokoni Julai 24, 2024.

Baada ya miezi kadhaa ya kujiridhisha, kampuni ya vifaa vya kielektroniki ya Samsung imetangaza ujio wa pete hiyo itakayouzwa kwa Dola 399.99 za Marekani (sawa na Sh1,073,928 za Kitanzania).

Kampuni hiyo ilizindua kifaa hicho kwenye hafla yake ya ‘Galaxy Unpacked’ jana Jumatano, Julai 10, 2024 kama nyongeza ya hivi punde kwenye mfumo wake wa ikolojia wa vifaa ambayo inasema vinaendeshwa zaidi na akili ya bandia (AI).

Pete hizo zinatengenezwa kwa malighafi tofauti, kwani zipo za madini ya dhahabu, fedha na nyeusi.

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, pete hiyo ina kifaa kinachoweza kufuatilia harakati za mtu wakati wa usingizi, muda wa kulala, mapigo ya moyo na kupumua na kutoa uchambuzi wa ubora wa usingizi.

Samsung imesema pete hiyo pia inatumia joto la ngozi, ili kufuatilia mzunguko wa hedhi wa mwanamke na kumpa taarifa.

Pia mlio wa pete hiyo unawafahamisha watumiaji wakati mapigo yao ya moyo yanapoongezeka au kuwa chini isivyo kawaida. Watumiaji wanaweza pia kuangalia mapigo ya moyo wao katika muda halisi.

Pete hiyo ina uwezo wa kutambua aina ya mazoezi au shughuli ambayo mtu anafanya na kumpa mrejesho, iwapo ametembea umbali gani na kuchoma karolisi kiasi gani.

Kwa mujibu wa Samsung, pete hiyo ina uzani wa kati ya gramu 2.3 na gramu 3, kulingana na saizi unayotaka kununua. Pia imesema betri ya pete hiyo inaweza kudumu hadi siku saba. Kuna kipochi cha kuchaji kinachobebeka, kama vile vipuli vya hewa visivyo na waya.

Pete hiyo itakayotumia vihisia vidogo kufuatilia vipimo mbalimbali vya afya, hadi sasa zimekuwa bidhaa muhimu

Related Articles

Back to top button
Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker!