NewsSWAHILI NEWS

Aliyekuwa RC Simiyu kizimbani kwa tuhuma za ulawiti

Dar es Salaam. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dk Yahaya Nawanda amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mkoa wa Mwanza na kusomewa shtaka moja la kulawiti.

Dk Nawanda amepandishwa kizimbani leo Jumanne Julai 9, 2024, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Mkoa wa Mwanza, Erick Marley na kusomewa shtaka hilo na waendesha mashtaka wa Serikali, Magreth Mwaseba na Martha Mtiti.

Kwa mujibu wa Mwaseba, mshtakiwa (Nawanda) alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 154 (1)(a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu sura ya 16.

“Mshtakiwa, Yahaya Nawanda, Mkazi wa Nyamata wilayani Bariadi mkoani Simiyu unashtakiwa kwa kosa la kumwingilia kinyume na maumbile’kumlawiti’ Tumsime Ngemela kosa ulilolitenda Juni 2, 2024 eneo la maegesho ya magari lililoko Rock City Mall wilayani Ilemela mkoani Mwanza,” amesema Mwaseba.

Related Articles

Back to top button
Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker!