NewsSWAHILI NEWS

Aliyechoma picha ya Rais aachiwa, awashukuru Watanzania

Dar es Salaam. Msanii wa Sanaa ya uchoraji, Shadrack Chaula (24) ameachiwa huru leo Jumatatu Julai 8, 2024 baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kushindwa kulipa fidia ya Sh5 milioni kwa kosa la kutoa taarifa za uongo mtandaoni.

Julai 4, 2024 Chaula aliyekamatwa kwa madai ya kuchoma picha ya Rais Samia Suluhu Hassan na kushtakiwa kwa kosa la kutoa taarifa za uongo, alihukumiwa katika Mahakama ya Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya, baada ya mshtakiwa huyo, mkazi wa Kijiji cha Ntokela, wilayani humo, kukiri kosa hilo.

Hata hivyo, watumiaji wa mtandao wa X (zamani Twitter) walichanga faini hiyo kwa ajili ya kumtoa. Kupitia ukurasa wa Instagram wa Wakili Peter Kibatala amewashukuru wote waliochangia.

“Kama inavyoweza kuthibitishwa na picha; Shadrack Yusuph Chaula yuko huru mmelipia uhuru wake; na uhuru wa maoni katika nchi hii,”ameandika Kibatala aliyeambatanisha na picha ya Chaula wakiwa pamoja.

Related Articles

Back to top button
Close

Adblock Detected

Please consider supporting us by disabling your ad blocker!